Thursday , 1st Nov , 2018

Wasomi mbalimbali nchini ambao wameshiriki kongamano la kujadili hali ya uchumi na siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano, Profesa wamependekeza kutumika kwa lugha ya Kiswahili kwenye taasisi zote za shule nchini.

Profesa Martha Qorro

Mmoja wa wadau hao ni Profesa Martha Qorro ambaye ametoa kauli hiyo katika kongamano ambalo limehudhuriwa na watu mashuhuri mbalimbali, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt Bashiru Ally, Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamaba Kabudi, Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba.

Profesa Martha amesema “napendekeza Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia kwa ngazi zote wasomi tunaovyongea kingereza huwa tunajitenga na jamii lazima watu wakitumwa kusoma nje wanapaswa kuja kututafsiria waliyojifunza kwa lugha ya Kiswahili, lakini sidhani kama hili limewahi kufanyika

Aidha Profesa Martha ambaye ni mwanamke pekee aliyetoa mada kwenye kongamano hilo amesema tafiti nyingi zinazofanywa na baadhi ya wasomi nchini zimekuwa haziendani na uhalisia wa maisha ya lugha ya mtanzania.

Vyuo Kikuu vinafanya tafiti nyingi sana lakini ukizichukua na kuzipeleka mtaani hakuna mtu atakayeelewa” Amesema Profesa Martha Qorro