Tuesday , 22nd Jul , 2014

Viungo mbali mbali vya binadamu vimekutwa katika eneo la kutupa taka la Bunju jijini Dar es Salaam katika mazingira ambayo haijafahamika mara moja kuwa viungo hivyo vimetoka wapi.

Mkuu wa Polisi mkoa wa Kinondoni kamanda Camilius Wambura.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni Camelius Wambura amesema viungo hivyo vya binadamu vilivyokutwa ni miguu na vidole ambavyo vilikutwa vikiwa vimefungwa ndani ya mifuko.

Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo lililobeba viungo hivyo vya binadamu.

Jeshi la polisi ilibidi litumie nguvu ya ziada kwa kufyatua mabomu ya machozi kutawanya umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika kituo kidogo cha polisi cha Bunju Usalama, ambako gari lililobeba baadhi ya viungo hivyo lilikuwa likishikiliwa kwa muda.

Tukio hilo limevuta hisia kubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo kadhaa nchini, huku kukiwa na utata kuhusu idadi kamili ya viungo hivyo pamoja na chanzo chake.