Mashindano ya kucheza muziki ya Dance 100% 2014 DSM Tanzania
Kama una crew yako ya watu wanne hadi nane kutoka pande zote za Tanzania, mnatakiwa kufika kwa ajili ya usaili huo wa pili utakaofanyika kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa sita mchana.
Safari ndio inazidi kupamba moto huku wote tukitaka kujua nani atakuwa King wa Dance100% 2014 na kuondoka na kitita cha shilingi milioni Tano za Tanzania.
Kumbuka usaili huo wa pili utafanyika viwanja vya basketball vya Don Bosco Oysterbay vilivyopo karibu na kituo cha mabasi Mbuyuni na pia karibu na maduka ya Namanga.
Mashindano hayana kiingilio chochote..tukutane pale Don Bosco Oysterbay Jumamosi hii, jipange.