Monday , 21st Jul , 2014

Wanamuziki wa miondoko ya muziki wa injili wameendelea kujitokeza kumsindikiza mwimbaji nyota wa Rose Muhando katika uzinduzi mkubwa wa albamu yake mpya aliyoibatiza jina ‘Kamata Pindo la Yesu’.

Mwimbaji muziki wa injili nchini Rose Mhando

Uzinduzi huo ambao utahudhuriwa na mgeni rasmi Waziri Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye utasindikizwa na wanamuziki maarufu wakiwemo Upendo Nkone, John Lissu, Bonny Mwaitege na Ephraim Sekeleti.

Muandaaji wa tamasha la uzinduzi huo Alex Msama ameelezea kuwa bado wanamuziki wengine wanaendelea kujitokeza kwa ajili ya uzinduzi huo ambao utafanyika Agosti 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam.