
Yanga walio katika mashindano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi, wanamuhitaji mshambuliaji huyo ili kuboresha safu yao ya ushambuliaji inayoonekana kutetereka kwa hivi sasa baada ya kuondoka kwa Donald Ngoma na majeraha ya Amisi Tambwe.
Aidha tetesi zinaeleza kuwa, Yanga wanamfukuzia kimya kimya mshambuliaji huyo huku wakitanabaisha kuwa staa huyo amebakiza mwezi mmoja tuu katika mkataba wake na mabingwa hao wa Kenya Gor Mahia.
Kagere alikuwa gumzo katika mashindano ya Sportpesa Super Cup yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini Kenya huku akiwaadhibu Simba katika mchezo wa fainali kwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0.