Sunday , 6th Jul , 2014

Akiwa amejiunga na Lebo maarufu ya muziki nchini Kenya Calif Records msanii ambaye pia ni muigizaji filamu nchini Kenya Doris Achieng aka Dohr ameendelea kung'aa katika chati baada ya kutoa wimbo wake mpya alioubatiza jina "Nimechoka".

Msanii na mwanamitindo wa Kenya Doris Achieng

Dohr mwenye umri wa miaka 21 amekuwa ni msanii wa kike ambaye hivi sasa amefanya kolabo na wasanii wakali nchini humo kama Mejja, Ala C na Alpha, yupo mbioni kutoa traki mpya na msanii Jimwat.

Dohr pia ni mwanamitindo ambaye amefanya modeling katika makampuni mbalimbali na pia aliwahi kushine katika onesho kubwa la 'Support Women Art in Kenya' (SWAN).