Waziri wa Fedha wa Singapore, Heng Swee Keat , ametangaza hatua hiyo wakati akiwasilisha Bungeni Bajeti, ambapo amesema, bonasi hiyo ni dhamira ya muda mrefu ya serikali ya kugawana matunda ya maendeleo na raia wake.
Waziri huyo amesema, takriban watu milioni 2.7 watalipwa bonasi hiyo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Amesema wale wenye kipato cha kuanzia Dola ya Singapore elfu 28 watalipwa bonasi ya Dola 300 na wale wenye kipato cha kati ya Dola 28,001 hadi Dola laki moja watalipwa bonasi ya dola 200.
Mnamo mwaka 2011, watu wazima nchini humo waliokuwa na kipato cha mwaka cha hadi dola elfu 30 walilipwa bonasi ya dola 800.
