Wednesday , 7th Feb , 2018

Jumatatu tuliwaletea historia fupi ya Mfalme Mswati wa Swaziland na wake zake, na leo inaendelea kwa wake waliosalia ambao hawakuandikwa. Wasome kwa makini kuwajua, yupo binti aliyeacha shule, yupo aliyefumaniwa na kipenzi cha Mfalme.

Mke wa 6, Inkhosikati LaMagwaza, huyu ni mpenda sanaa, aliolewa na mfalme Mswati mwaka 1993, aliamua kumuacha mfalme kwa skendo ya kuchepuka baada ya kuwepo taarifa za kuwa na mahusiano na kijana wa Afrika Kusini, baadaye mahusiano hayo aylikuja kufa na badaye kuolewa na mfanyabiashara maarufu wa Afrika Kusini.

Mke wa 7, Inkhosikati LaMasango ,  Huyu aliolewa mwaka 2000 na King Mswati, kabla ya hapo alishawahi kufukuzwa shule mbili tofauti kwa utovu wa nidhamu, baada ya hapo aliamua kuacha kusoma na kuanza kujihusisha na sanaa ya kuchora ambayo ilimpa mafanikio makubwa, na kufanya shughuli za kusaidia jamii kupitia sanaa yake.

Mke wa 8, Inkhosikati LaGija, huyu aliolewa mwaka 2002, alikuwa mwanamke wa 3 kumuacha Mfalme ambapo mwaka 2012 alikimbia. La Gija alikimbilia Afrika Kusini na kumuacha mtoto wake wa kike. Tetesi zinasema kuwa mume wake alikuwa akimtesa sana na ndio sababu ya kukimbia.

Mke wa 9,  Inkhosikati LaMagongo, huyu aliolewa mwaka 2002, na miongoni mwa wanawake vipenzi wa Mfalme Mswati, Lamagongo ni maarufu kwa michezo tangu akiwa shule, na alishawahi kusikika kwenye vyombo vya habari akisema kuwa UKIMWI unaweza ukaingia Ikulu, lakini iwapo itatokea hatojali kwani anamuamini sana Mungu na yeye bado kijana, hivyo hawezi kuishi kwa ofu.

Mke wa 10, Inkhosikati LaMahlangu, huyu aliolewa mwaka huo huo 2002 tena alichukuliwa kinguvu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Swaziland zinasema kuwa mama wa mtoto huyo aligundua binti yake alitoweka shuleni, na alipewa taarifa kuwa wanaume wawili walimchukua na kumpeleka kwa Mfalme, alienda kutoa taarifa polisi lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, na baadaye watu walimfuata na kumueleza kuwa binti yake yupo kwa Mfalme na amepangiwa majukumu ya Kifalme, alihangaika kuhakikisha mtoto wake anarudishwa lakini imeshindikana na mpaka leo bado yupo kama mke wa Mfalme Mwsati.

Mke wa 11, : Inkhosikati LaNtentesa, huyu aliolewa mwaka 2005 kwa sherehe ya kimila, ni Matron wa kituo kimoja cha watu wasio n uwezo na wenye matatizo, anaelezwa kuwa mtu asiye na makeke.

Mke wa 12,  Inkhosikati LaDube, huyu aliolewa akiwa na miaka 16, ni miongoni mwa wanawake warembo wa kasri ya Mfalme Mswati, LaDube alikumbwa na skendo ya ngono baada ya kufumaniwa na waziri wa sheria wa nchini humo. Baada ya hapo alifungwa kifungo cha nyumbani cha zaidi ya mwaka, lakini taarifa zinasema kwamba alifukuzwa kwenye kasri ya Swaziland.

Mke wa 13, Inkhosikati LaNkambule, huyu aliolewa mwaka 2007 na amezaliwa mwaka 1990, anajulikana kama 'The Young and Restless queen'. Kitaaluma ni mtangazaji wa televisheni, alichaguliwa kwa ngoma maalum ambayo huchezwa kwa ajili ya mfalme kuchagua mke akiwa na miaka 17, muda mfupi baada ya Mfalme Mswati kupiga marufuku kwa binti kuolewa kabla ya miaka 18.

Mke wa 14, Sindiswa Dlamini, huyu aliolewa mwaka 2013, kwenye sherehe ya mfalme kuchagua mke, akiwa bado binti mbichi na aliyehitimu high school mwaka uliopita. Mpaka sasa yupo na Mfalme na anatajwa kuwa miongoni mwa wake vipenzi wa Mfalme Mswati

Mke wa 7, Inkhosikati LaMasango
Mke wa 8, Inkhosikati LaGija
 Inkhosikati LaMagongo
Inkhosikati LaMahlangu,
Inkhosikati LaNtentesa
Inkhosikati LaDube aliyefumaniwa
Inkhosikati LaNkambule aliyekuwa Mtangazaji wa Televisheni
Sindiswa Dlamini