Submitted by Anonymous on Monday , 16th Jun , 2014
Rich Mavoko akiwa na washeza shoo wake wakiwa wamekaa backstage wakisubiria kupanga kwenye jukwaani.
Kundi la Weusi na Jambo Squad wakiwa kwenye picha ya pamoja backstage.
Kundi la Weusi na Jambo Squad kabla ya kupanda kwenye jukwaa la Kili Music Tour ndani ya mji wa Kahama.
Umati mkubwa wa wakazi wa Kahama uliojitokeza na kufurahia tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Kahama.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Shilole a.k.a Shishi Baby akiwapagawisha wakazi wa Mji wa Kahama.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Shilole a.k.a Shishi Baby akinengua jukwaani.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Rich Mavoko akiwajibika jukwaani.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Rich Mavoko akiwajibika jukwaani huku akisindikizwa na wacheza shoo wake.
Umati mkubwa wa wakazi wa Kahama uliojitokeza na kufurahia tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014. Wakazi wa kahama wakishangiria burudani toka kwa wasanii mbalimbali.
Wasanii wa Kundi la Jambo Squad toka Jijini Arusha wakiwasha moto kwenye jukwaa la kili music tour ndani ya Kahama.
Wasanii wa Kundi la Jambo Squad toka Jijini Arusha wakiwapagawisha wakazi wa Kahama wakati wa tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Kahama.
Wasanii wa Kundi la Jambo Squad juu ya jukwaa la kili music tour kahama.
Msanii wa muziki wa dansi, Christian Bella akitoa burudani kwa wakazi wa Kahama.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Ay akiwapa burudani ya aina yake wakazi wa mji wa Kahama wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Kahama.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, MwanaFA akiwachezesha bila kukunja goti wakazi wa mji wa Kahama wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014.
Mwana FA na AY wakitoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wao wa Kahama.
Wasanii wa Kundi la Weusi linaloundwa na Joh Makini, Nikki 2, G-Nako toka Jijini Arusha wakifanya onyesho la aina wakati wa wa tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Kahama.
Wasanii wa kundi la Weusi Nikki 2 na G-Nako wakiwapa burudani wakazi wa Kahama.
Kundi la Weusi wakitoa burudani kwa wakazi wa Kahama wakati wa shangwe za Kili Music Tour 2014.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akizungumza na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Bugozi Musuguri katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es salaam tarehe 01 Novemba 2024.