Wednesday , 5th Jul , 2017

Kamishna wa ufundi na Uendeshaji mashindano wa Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Manasseh Zablon amezitaka timu shiriki katika michuano ya Sprite BBall Kings kuongeza juhudi na heshima ya mchezo huo ili waweze kutimiza malengo yao.

Kamishna wa ufundi na Uendeshaji mashindano wa Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Manasseh Zablon.

Manasseh ameeleza hayo muda mchache baada ya kumalizika kwa droo ya 'Live' ya nne na ya mwisho ya kupanga ratiba ya mashindano hayo yaliyofanyika katika ofisi EATV LTD Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

"Katika hatua ya 'semi final' ya michuano ya BBall Kings tunaongeza vionjo kwa upande wa waamuzi badala ya kuchezesha wawili sasa hivi tutakuwa na watatu pia tutatoka nje zaidi kwenye viwanja vya kuchezea mchezo huu", alisema Manasseh.

Pamoja na hayo Manase ameendelea kwa kusema "mtu ukifungwa mechi mbili mfululizo ina maana 'game'imekishwa na ukifungwa moja, ukashinda moja itabidi ucheze 'final game'moja ambayo ndiyo itakuwa imeamua ni timu gani iweze kuingia katika hatua ya fainali moja kwa moja. Kwa hiyo nizitake timu shiriki ziongeze 'discpline' ili watu waweze kujionea radha nzuri ya mchezo huu ambao kwa sasa EATV LTD wanarudisha heshima ya mpira wa kikapu baada ya kupotea kwa kipindi kirefu", alisisitiza.

Kwa upande mwingine, Manasseh amesema katika hatua hii ya nusu fainali ana imani kubwa kwamba ushindani utaongezeka maradufu kwa kudai timu zilizoingia zote zipo vizuri na uwezo wa hali juu.