Saturday , 31st May , 2014

Jose Chameleone, amezungumzia sakata la ugomvi unaoendelea kati ya Moze Radio na Jeff Kiwa baada ya kupata taarifa akiwa ziarani Brussels, na kusema kuwa kwa nafasi yake hawezi kuchukua upande wala kutoa maoni yoyote kutokana na yeye kuwepo mbali.

Jose Chameleone katika show ya Moze na Weasel

Chameleone amesema kuwa, akiwa kama kaka anayewatakia mema Radio na Weasel katika safari yao kimuziki, anajisikia vibaya kuona wanapitia katika changamoto hii ya ugomvi na anawatakia kumaliza sakata hili salama.

Sababu mbalimbali zimekuwa zikitajwa kuwa ndio chanzo cha ugomvi wa Jeff na Moze Radio, mojawapo ikielezwa kuwa ni kitendo cha Jeff kuropoka kuwa, Moze si baba halisi wa mtoto ambaye msanii huyu amezaa na mwanamuziki Lilian Mbabazi.