Wednesday , 28th May , 2014

Mwanamuziki wa dansi nchini Tanzania Christian Bella ameeleza kuwa yeye ni miongoni mwa wanamuziki watakaopanda jukwaani Jumamosi hii katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza katika ziara ya muziki ya Kili Tour.

Bella amelazimika kutoa ufafanuzi huo alipoongea na eNewz juu ya habari ambazo zimekuwa zikiwachanganya mashabiki haswa wa mkoani Mwanza kwamba mwanamuziki huyo hatopaform katika Uwanja wa CCM Kirumba siku ya Jumamosi.

Mkali huyo amewaondoa hofu mashabiki wake wote kuwa lilitokea tatizo la utoaji habari za tarehe na siku ya onesho la bendi yake ambayo nayo ipo ziarani mkoani humo, hivyo Jumamosi ya tarehe 31 mwezi huu Bella atafanya makamuzi yake kama kawaida ndani ya uwanja wa CCM Kirumba.