
Mbishi amefunguka kwenye Planet Bongo ya East Africa radio wakati akipiga story tatu na kusema kwamba hajawai kutoa wimbo mbaya na ndiyo maana anaendelea kudumu kwenye 'game' huku akikutana na changamoto, na kuongeza kuwa tasnia imegeuka na kuwa ya familia ndiyo sababu yeye amekuwa mwanaharakati wa kuikomboa.
Nikki amedai kwamba "Napata challenge na nnachokifanya, naonekana chizi, watu wanasema kwamba sifanyi muziki mzuri nazungumzia game. wapo wanaongea maneno mabaya sana na wengine wanakoment kwenye mitandao ya kijamii kwamba nitakuja kushtuka kuwa muziki ulikuwa unalipa nikishazeeka, mimi nawajibu sina muziki mbaya"- Nikki Mbishi.
Aidha Mbishi amezidi kufunguka na kutoa mifano kwamba kuwa na maneno ya busara hakumaanishi kutamfanya tajiri kwani kina Mandela walizungumza maneno ya busara lakini bado hawakufikia utajiri wa Billgate na ndivyo ilivyo hata kwenye mashairi yake
Msikilize Mbishi hapa chini akidadavua zaidi.