Tuesday , 9th May , 2017

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametoa magari matatu mapya ya kubebea wagonjwa kwa wabunge watatu ili kuwasaidia wananchi wa maeneo yao ya ubunge.

Rais Mgufuli

Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amekabidhi magari hayo kwa niaba ya Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mkoa wa Rukwa Mhe. Ally Keissy, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora Mhe. Munde Tambwe na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga.