
King Zillah
King Zillah amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema hakuna rapa ambaye anaweza kufanya mitindo huru kama yeye, Zillah anasema kigezo alichotumia ni kutokana na baadhi wa rapa kupewa nafasi ya kuonesha uwezo wao ndani ya dakika kumi za maangamizi ndani ya Planet Bongo, huku yeye akizitumia dakika zote kumi kufanya mitindo huru tofauti na wengine.
"Naamini wewe mwenyewe unajua kuwa mimi ni mfalme wa 'freestyle' hata ile dakika kumi za maangamizi pia zimeleta jibu juu ya hili, lakini pia utofauti wangu natengeneza freestyle na hits" alisema King Zillah
Mbali na hilo Rapa Young Killer jana alifunguka na kusema kwa bongo yeye anamkubali zaidi Godzillah pamoja na Nikki Mbishi kwa 'freestyle' pia alikuwa akimuelewa marehemu Albert Mangwea na kusema hajawahi kumkubali Fid Q kwa 'freestyle' sababu hajawahi kumuona akifanya kitu hicho.
Zitazame hapa dakika kumi za maangamizi za King Zillah, Fid Q, Nikki Mbishi, Young Killer pamoja na Chemical