Monday , 23rd Jan , 2017

Rapa Madee leo amefunguka na kutaja wasanii wa Hip hop watano ambao anawakubali na anapenda kuwasikiliza mara kwa mara na kusema mtu wa kwanza ambaye yeye siku zote huwa anapenda kazi zake pia huwa anapenda kupata ushauri wake siku zote ni Fid Q.

Madee (Kushoto) akiwa na Fid Q ndani ya FNL ya EATV

Madee anasema ukimtoa Fid Q wasanii wengine ambao anawakubali na kupenda kazi zao kutoka Bongo ni pamoja na Mzee wa Dume Suruali Mwana FA, Mr Blue, Roma Mkatoliki pamoja na God Zillah.

Mbali na hilo Madee anasema yeye amejiwekea utaratibu wa kubadili aina ya muziki wake kila baada ya miaka mitano, ili kwenda sawa na soko la muziki la wakati huo na kusema ameamua kufanya hivyo sababu muziki wa sasa unahitaji ujanja ujanja ili mambo yaweze kwenda.