
Mzee Majuto
Akiongea na EATV Mzee Majuto alisema kuwa yeye hawezi kukubali kuona fani inachezewa chezewa na watoto hivyo ataendelea kuigiza mpaka siku atakayokufa kwa sababu uwezo wake ni wa hali ya juu kwenye kuandika na kuigiza.
"Kuigiza kwangu ni kama maradhi vile hivyo sidhani kama naweza kuacha, siwezi kukaa pembeni sanaa ikawa inachezewa na watoto sitaki kabisa nasema hivi mimi nitaendelea kuigiza mpaka nakufa". Mzee Majuto