Saturday , 10th Dec , 2016

Mkongwe katika anga za bongo fleva, Dully Sykes amekutana na maajabu katika usiku wa Tuzo za EATV na kutangaza rasmi kuwa mwakani na yeye lazima ashiriki kwa kuwa atakuwa na vigezo vyote vinavyohitajika.

Dully Skykes muda mfupi baada ya kuwasili

Dully ambaye ni mkali wa ngoma ambayo inasumbua kila kona ya Afrika Mshariki, inayokwenda kwa jina la Inde, amefunguka hayo baada ya kuwasili na kushangazwa na maandalizi aliyoyakuta katika usiku wa tuzo, uliofanyika Mlimani City Dar es Salaam.

Dully amepongeza EATV kwa kuanzisha tuzo hizo, na kukiri kuwa siku ya leo amekutana na mambo ambayo hajawahi kuyaona yakifanyika nchini Tanzania tangu aingie kwenye muziki.

Akielezea wimbo wake wa Inde kutoshiriki mwaka huu, Dully amesema mwaka huu wimbo huo haukuwa na vigezo kwa kuwa ulikuwa umetolewa nje ya muda wa tuzo, lakini mwakani utakuwa na sifa zote, na anaamini ataondoka na tuzo.

Tags: