Wednesday , 7th Dec , 2016

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda Maurice Kirya anatarajiwa kupanda jukwaa la EATV AWARDS 2016 kwa mara ya kwanza na kuandika historia ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Uganda kuperfom kwenye tukio kubwa katika tasnia ya muziki Afrika Mashariki

Mourice Kirya

Msanii huyo ambaye ni mkali wa kucharaza nyaya za gitaa na sauti yake ya kuvutia kwenye muziki wa R&B, ataongozana sambamba na mkali mwingine kutoka Tanzania, ambaye ni fundi wa kutengeneza muziki na mwenye sauti ya ajabu, Barnaba Classic.

Barnaba Classic

Barnaba ambaye pia amedhamiria kufanya show kali na kuandika historia, hivi sasa anatamba na nyimbo zake kama lover boy na wanaifaa, licha ya nyingine ambazo zimekuwa haziishi muda masikioni mwa wasikilizaji na kufanya msanii huyo kuendelea kuwa fundi kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva

Mtazame hapa Mourice Kirya katika ngoma yake ya Ghost 

Tags: