Saturday , 3rd Dec , 2016

Mtangazaji maarufu wa runinga ambaye ni rafiki na kipenzi cha wengi Salama Jabir ataandika historia sambamba na kampuni EATV LTD baada ya kupata nafasi ya kipekee ya kuwa 'HOST' wa tuzo za kwanza za EATV

Sherehe hizo za utoaji wa tuzo ambazo ni kubwa zaidi Afrika Mashariki na zinafanyika kwa mara ya kwanza , zitatolewa Desemba 10, 2016 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam

Baada ya East Africa Television LTD kumtangaza Salama Jabir mwenyewe alionyesha kufurahia na alitumia akaunti yake ya Twiiter kuweka ujumbe maalum wa kuonesha furaha yake

Wadau mbalimbali nao hawakuwa nyuma kuonesha  shangwe zao kwa kufurahia habari njema ambayo kwa sasa ndio gumzo la Afrika Mashariki, huku wakiandika hisia zao na kutoa pongezi.

Maoni ya watu baada ya EATV kumtangaza Salama Jabir kuwa HOST wa #EATVAwards
Tags: