
Akizungumza na Hotmix Michezo, Mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa chama cha mpira wa wavu mkoa wa Dar es salaam DAREVA, Nassoro Shariff amesema mpaka sasa ni timu saba pekee zilizohakiki ushiriki huo lakini wanaamini mpaka ifikapo Novemba 27 watapata timu nyingi zaidi shiriki za mashindano hayo yenye lengo la kuandaa timu kuelekea katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kufanyika Januari mwakani visiwani Zanzibar.
Shariff amezitaka timu kuendelea kujitokeza kwa ajili ya kuhakiki ushiriki wa mashindano hayo ambayo ni ya wazi ili kuweza kupata timu nyingi shiriki zitakazoleta ushindani katika mashindano hayo.