
Alfred Lucas - Afisa habari TFF
Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa vilabu hivyo vinapaswa kukamilisha zoezi hilo kabla ya Novemba 30 mwaka huu huku akiwataka pia wamiliki wa vilabu shiriki vya ligi kubadili umiliki wa vilabu ndani ya muda huo.
Alfred amesema, iwapo klabu hizo mbili zitakuwa hazijamaliza kujaza fomu hizo ambazo zitaonesha majina ya wachezaji walio ndani ya klabu pamoja na benchi la ufundi hazitapata leseni na zitakuwa katika hatari ya kutoshiriki katika michuano hiyo.
Alfred amesema, kwa upande wa wamiliki wa vilabu, wametakiwa kuhakikisha kuwa kila timu inakuwa na mmiliki mmoja ambaye haruhusiwi kumiliki timu mbili zilizo ndani ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.