
Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako
Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa kuelimisha wanafunzi juu ya masuala ya rushwa, maadili pamoja na utekelezaji wa haki za binadamu na utawala bora iliyoandaliwa na taasisi na mashirika ya serikali ya kupambana na rushwa, uwajibikaji na utawala bora
Valentino Mlowola - Mkurugenzi TAKUKURU
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini Tanzania Bw. Valentino Mlowola amesema ofisi yake ipo katika mkakati wa kuandaa mtaala kwa ajili wa kufundishia wanafunzi kuanzia shule za msingi hadi vyuoni utakaotumika kutoa elimu kuhusu rushwa ili kujenga taifa lenye kufuata maadili na kukataa rushwa.