Sunday , 13th Nov , 2016

Taifa Stars leo itashuka dimbani mjini Harare, Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zimbabwe.

Wachezaji wa Stars walipokuwa wakifanya mazoezi kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini DSM kujiandaa na mchezo dhidi ya Zimbabwe utakaochezwa leo.

Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwassa ameahidi ushindi mkubwa kwani wachezaji wake wote wametoka kwenye ligi wakiwa na nguvu.

Kikosi cha Taifa Stars chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ni Makipa Deogratius Munishi na Aishi Manula, Mabeki ni Erasto Nyoni Michael Aidan, Mwinyi Haji, Mohamed Hussein na Vicent Andrew.

Viungo wa Kati ni Himid Mao, Mohammed Ibrahim, Jonas Mkude na Muzamiru Yassin na wale wa pembeni ni Shiza Kichuya, Simon Msuva na Jamal Mnyate na washambuluaji ni Ibrahim Ajib, John Bocco, Mbwana Samatta, Elius Maguli, Thomas Ulimwengu na Omar Mponda. Mchezo huu utakuwa na faida zaidi kwa Tanzania kama ikiwafunga Wazimbabwe.