Sunday , 30th Oct , 2016

Jukwaa la Wahariri limehuzunishwa na hatua ya kamati ya bunge ya maendeleo ya jamii inayosisitiza kuendelea kuufikisha bungeni muswada tata wa habari ambao wadau wakiwemo wanahabari wameulalamikia kuwa na mapungufu yatakayodidimiza fani ya uandishi.

Viongozi wa Jukwaa la Wahariri - TEF katika mkutano wao na wanahabari jijini Dar es Salaam leo

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bw. Teophil Makunga ameiomba serikali pamoja na bunge kuwasilisha muswada huo katika kikao cha bunge cha mwezi Februari mwakani ili kutoa muda kwa wadai kuwasilisha maoni yao kuhusu muswada huo.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bw. Deodatus Balile ameshangazwa na Kamati hiyo kuegemea maoni ya waalikwa na kuyafanya ndio maoni halisi huku ikiwaacha wadau muhimu katika muswada huo kama wanahabari pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari.