Monday , 24th Oct , 2016

Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Nyota Africa ya Morogoro na  timu ya Mkoa wa Morogoro CRESENCE BANZI amefariki dunia na kuzikwa leo kwenye makaburi ya Kola yaliyopo Manispaa ya Morogoro.

Ramani ya Morogoro

Marehemu BANZI wakati wa uhai wake alikuwa mpenzi wa soka na alifanikiwa kuchukua kombe la Taifa mwaka 1970 mkoani Morogoro, ambapo aliendelea kuichezea timu ya mkoa wa Morogoro mpaka mwaka 1972.

Marehemu alianza kuugua ugonjwa wa maumivu ya mgongo, tangu tarehe 29/9/2016, ambapo  alipelekwa  kwenye hospitali ya Muhimbili jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya matibabu, lakini tarehe 22/09/2016 marehemu  aliaga dunia.

Pia marehemu banzi amefariki akiwa na umri wa miaka 68 huku akiwa ameacha mke na watoto watatu pamoja na wajukuu 8.