Friday , 2nd Sep , 2016

Msanii Beka Ibrozama amezizungumzia tuzo za muziki na filamu kwa Afrika Mashariki, EATV AWARDS, na kusema zimeleta changamoto kwao.

Beka

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Beka amesema tuzo hizo ambazo ni kubwa na zitaleta changamoto kubwa kwa wasanii kufanya kazi zenye ubora, zitakazomuwezesha kupata tuzo hiyo, ambayo anaitabiria kufanya makubwa kwenye tasnia ya sanaa ya muziki na filamu nchini.

“Tuzo zimeleta chalenge kubwa sana kwetu, kwa sababu watu watakuwa wanafanya kazi, ili mtu anajua kazi yangu hii ikiingia kwenye tuzo, basi nikikosa huku nitapata huku, na sisi tutasema yah hiki ndio kitu tulichokuwa tunakitaka”, alisema Beka.

Beka aliendelea kusema kwamba ana imani tuzo hizo zitakuwa na ubora ule unaofaa, ukizingatia vigezo vya kazi za sanaa na kuzipa tuzo kadri inavyostahili na uhalisia wake.

Tags: