Friday , 2nd May , 2014

Bingwa wa zamani wa dunia kwenye mchezo wa Chess Grand Master Gary Kasparov amesifu jutuhada zinazooneshwa na chama cha mchezo huo nchini Uganda (UCF) katika kuukuza mchezo huo.

Gary Kasparov, akicheza Chess

Bingwa wa zamani wa dunia kwenye mchezo wa Chess Grand Master Gary Kasparov amesifu jutuhada zinazooneshwa na chama cha mchezo huo nchini Uganda (UCF) katika kuukuza mchezo huo hasa miongoni mwa vijana.

Kasparov ametoa kauli hiyo leo wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili nchini humo ambayo ameifanya kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa chama cha mchezo huo duniani (FIDE) utakaofanyika mezi wa nane mwaka huu nchini Norway.

Raia huyo wa Urusi amecheza michezo 11 na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambapo ameshinda michezo yote, baadhi yake ikiwa ni dhidi ya wanafunzi wa shule ya msingi St Joseph, Kagoma Gate na Trinity College Nabbingo.