Wednesday , 30th Apr , 2014

Mwanasiasa Mhe. Halima Mdee ambaye ni mbunge wa Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam, leo hii ameshiriki katika kipengele cha Kikaangoni Live cha ukurasa wetu wa facebook, ambapo wapenzi wa ukurasa huu wameweza kumuuliza moja kwa moja maswali.

Mhe. Halima Mdee

Mhe. Mdee ameonyesha mapenzi makubwa aliyonayo kwa watu kwa kutumia muda wa saa mbili kujibu moja kwa moja maswali yao kibao ambayo wapiga kura wake pamoja na mashabiki wake 'wamemkaanga' nayo.

Mhe. Mdee amesema kuwa, amefurahi kupata nafasi ya kuchat na wananchi leo, kuwaelewesha juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea kisiasa na kijamii katika jimbo lake na mambo binafsi kwa wingi japo hakufanikiwa kujibu maswali yote.

Pia akagusia juu ya swala la wasanii anaowakubali ambapo katika orodha yake amewataja Weusi, Diamond, Ali Kiba, Mirror, Roma Mkatoliki, Kala Jeremiah, Lady Jay Dee na wengine wengi ambao amesema hangeweza kukamilisha orodha yao kwa mara moja.

Endelea kuwa sehemu ya familia kubwa ya wapenzi wa ukurasa wa facebook wa EATV, shiriki ukurasa huu na marafiki na Like pia kama bado hujafanya hivyo na kumbuka, Wiki ijayo tunakuletea mtu mwingine ambaye utachat naye moja kwa moja.