Buff G aka Buff G-Zinga amekuwa kimya kwa muda mrefu ameielezea enewz kuwa hii ni video mpya Ikiwa ni ujio mpya wa East Coast Team akiwashirikisha Snare, Gnako, na Lindah ambapo pia ameweka wazi mikakati yake mipya ya kibiashara zaidi kwa kuandaa kufungua label ya nguo inayokwenda kwa jina la GZINGA.
Buff G amesema kuwa anatarajia pia kutoa aina ya wine inayoitwa evesharone ambayo pia ipo katika hatua za majaribio na amewasihi mashabiki wake kuwa East Coast Team imerudi kwa kishindo huku ikianza mchakato wake wa kuanza kutambulisha wasanii wake wa zamani na wapya.