Akiongea mara baada ya kusaini makubaliaano hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile amesema kuwa kiasi cha shilingi bilioni 440 kitaelekezwa TASAF kwaajili ya kusaidia kaya masikini ikiwa ni pamoja na kusaidia ujenzi wa shule na upatikanaji wa ajira huku shilingi trilioni 1.9 kutengwa kwaajili ya miradi 10 iliyopitishwa na Benki ya Dunia.
Dkt. Likwelile amewataka wote watakaonufaika na miradi hiyo kuitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa ili kuweza kuleta maendeleo nchini.
Aidha kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird amesema kuwa hivi sasa benki ya dunia ipo katika majadiliano ya mwisho na serikali ya Tanzania ili waweze kutoa mkopo wa shilingi milioni 1,320 kwaajili ya ukarabati wa bandari ya Tanzania.



