
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Ahmed Msangi
Taarifa ya jeshi la polisi mkoani Mwanza imeeleza kuwa mnamo tarehe 15.06.2016 majira ya saa 8:20 mchana katika kijiji na kata ya Buhama tarafa ya Buchosa wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza, Ndimila Lupogosha miaka 30 mvuvi na mkazi wa kijiji cha Buhama aliuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na shingoni na mkewe aitwaye Martha Magugu miaka 40 pindi walipokuwa wakinywa pombe katika grocery ya mama Ali iliyopo katika kijiji hicho.
Inadaiwa kuwa tarehe 14.06.2016 majira ya saa 5 Usiku wakati wakinywa pombe katika grocery tajwa hapo juu, mke wa marehemu bi Martha alimuona mumewe akiongea na mwanamke mwingine kitendo ambacho hakikumfurahisha na kuamua kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani na shingoni hali iliyopelekea kutokwa na damu nyingi kichwani na kufariki dunia siku ya jana ya tarehe 15.06.2016 majira ya saa 8:20 mchana wakati akipelekwa hospitali, na baada ya kifo ndugu wa marehemu ndipo walipotoa taarifa polisi.
Chanzo cha mauaji inadaiwa kuwa wivu wa kimapenzi na mtuhumiwa wa mauaji hayo amekamatwa yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi, huku mahojiano dhidi ya tuhuma za mauaji anayodaiwa kutenda yakiendelea.
Pindi uchunguzi pamoja na upelelezi kuhusiana na tukio hilo ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani, mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi akiwataka kuwa makini wakati wote na maamuzi wanayoyachukua pindi wanapokuwa katika ugomvi ili kuweza kuzuia majeraha na vifo vinavyoweza kuepukika, kwani kujeruhi au kuua ni kosa la jinai hivyo jeshi la polisi litamshughulikia mhusika na kuhakikisha anafikishwa katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma zitakazo mkabali