
Waziri ameyasema hayo Bungeni wakati wa maswali na majibu ambapo waziri ametumia muda huo kuweza kutoa salamu zake kwa watoto wote nchini katika siku ya kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika Duniani.
''Kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi watoto 2358 wamebakwa katika kipindi cha mwaka jana kutoka watoto 422 mwaka jana hii inaonyesha kuwa idadi imeongezeka na kuashiria kwamba nyumba zetu siyo salama kwa watoto''- Amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha Waziri amesisitiza adhma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwalinda watoto dhidi ya ubakaji na kusema kuwa atakayebaka mtoto ajiandae kwa miaka 30 jela.