
Makamu wa Rais wa BFT Lukelo Wililo amesema, walikuwa na mashindano mawili katika nchi tofauti lakini kutokana na gharama wameamua kuchagua shindano moja ambalo wanaamini wataweza kufikia viwango.
Lukelo amesema, mashindano ya nchini Venezuela yanatarajiwa kufanyika Julai mwaka huu ambapo watachagua mabondia wa kwenda kushiriki mashindano hayo kutoka timu ya Taifa ambayo inaendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Lukelo amesema, kwa upande wa mabondia wa ngumi za kulipwa ni bondia Thomas Mashali ambaye mpaka sasa ndiye aliyejitokeza na emeshafanyiwa usajili kwa ajili ya ushiriki wa mashindano hayo.
Lukelo amewataka mabondia wengine we ngumi za kulipwa kupitia umoja wao kufanya mazungumzo na BFT ili kuweza kushiriki mashindano hayo ambayo yana umuhimu.
Lukelo amesema, timu ya Taifa ngumi za ridhaa inaendelea na mazoezi ikiwa na kocha mzawa huku ikisubiri kocha mwenye nyota tatu kutoka nchini Kenya kwa ajili ya kuongezea nguvu as kiufundi zaidi.
Lukelo amesema, wamemchukua kocha mwenye nyota tatu ili kuweza kuendana na hali ya sasa ya mchezo huo inavyotaka ya kuwa na makocha wa mchezo wa ngumi wenye nyota tatu.