Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenister Mhagama.
Wakizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika Mkoani Mbeya, wamesema kuna chama kipya ambacho kimeingilia matawi ya RAAWU, na kuchukua wanachama wake jambo ambalo ni kukiuka sheria zilizoanzisha vyama vya wafanyakazi nchini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini humo wamesema serikali ikiweza kudhibiti utitiri wa vyama hivyo utaweza kuondoa mkanganyiko unajitokeza unaofanya wafanyakazi wengine washindwe kufanya kazi zao.
Akizungumza nje ya Mkutano huo Katibu wa RAAWU, kanda ya kusini Bi. Mariam Mgalula amesema kuwa vyama vingi vya wafanyakazi vinakumbana na changamoto ya miundo na mfumo wa kuweza kuwasaidia wanachama wa vyama hivyo.
Bi. Mariam Mgalula amevitaka vyama hivyo kuhakikisha vinatetea maslahi ya wanachama katika suala zima la ajira na mikataba ikiwa ni pamoja na mishahara mizuri ambayo itawasidia wafanyakazi hao.