Wednesday , 23rd Apr , 2014

Mamlaka ya hali ya Hewa nchini Tanzania TMA imesema mikoa ya pwani nchini Tanzania itaendelea kupata mvua kubwa kwa siku kadhaa zijazo.

Akizungumza na East Africa Radia ,Kaimu Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa Dakta Hamza Kabelwa ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar es salaam,Tanga,Unguja na Pemba na kwamba kuna haja ya kuendelea kuchukua hatua kwa uwezekano wa kutokea mafuriko.

Dakta Kabelwa amefafanua kuwa mikoa mingine nchini itapata mvua za kawaida za masika ambazo sasa hivi ndiyo msimu wake.