Mashamba ya Migomba
Mansour ametoa kauli hiyo jijini Arusha mara baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa uliowakutanisha wataalamu wa utafiti wa kilimo kutoka taasisi na vyuo mbalimbali duniani.
Kaimu Mkurugenzi huo amesema kuwa bado kuna changamto nyingi katika uzalishaji wa zao la ndizi ikiwemo magonjwa hivyo wakulima wanatakiwa kulima kwa kutumia mbegu bora na za kisasa kwa lengo la kufanya kilimo cha biashara.
Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi inayoshughulikia taaluma ,utafiti,na ubunifu toka Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, Prof. Luganu Siluka amesema mkutano huo unahusisiha watalaamu wa uzalishaji ndizi wanaofanya kazi katika mradi unaoshughulikia uzalishaji wa ndizi.
Nae Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya kilimo cha Kitropical, ambao ndio watekelezaji wa mradi huo barani Afrika, amesema mradi huo unatekelezwa katika nchi mbili ambazo ni Tanzania na Uganda, kutoka na umuhimu wa zao hilo katika jamii ya nchi hizo.
Watalaamu hao kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wamekutana jijini Arusha kwa lengo la kupitia changamoto mbalimbali zinazololikabili zao la migomba na kutafuta ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kuelimisha mikakati ya namna ya kuongeza uzalishaji.