Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Askofu huyo amesema hayo wakatia akisimikwa kuwa askofu Mkuu Mwandamizi wa nne wa Kanisa hilo tangu kuanzishwa kwake na kwamba kanisa lao litakua bega kwa bega katika kusaidia maovu yanayofanywa na baadhi ya watendaji ambao sio waaminifu.
Askofu huyo amesema kuwa hatua anazozichukua Rais Magufuli ni jambo jema kwa watu wote lakini kuna baadhi ambao watakuwa wanachukia kutokana na matendo yao mabaya Watanzania wanatakiwa kumuombea ili kumlinda na maadui ambao watajitokeza katika harakati zake.
Hafla ya usimikaji wa Askofu huyo Mwandamizi imefanyika imefanyika katia viwanja vya kanisa kuu mjini Vwawa, mkoa mpya wa Songwe, ambapo mgeni wa heshima alikua Mkuu wa wilaya Mbozi, Ahmed Nammohe.
Akizungumza kwa niaba ya serikali Mkuu huyo wa wilaya amewataka viongozi hao wa dini waendelee kuhubiri amani na matendo mema ambayo yataisaidia nchi kutoka ilipo na kufika kule tunakotarajia kufika.