Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni ya UVCCM,na Mbunge wa viti maalumu kupita vijana Mkoani Kigoma, Zainab Katimba akiongea na waandishi wa habari
Akiongea mjini Kigoma Mbunge huyo wa viti Maalumu amesema kuwa hoja yake inalenga kushinikiza serikali itunge sera ya ulazima kwa taasisi mbalimbali kuajiri wahitimu wa elimu ya juu na ufundi ili kuwapatia mafunzo na hivyo kupata uzeofu ambao umekua kikwazo wakati wa kutafuta ajira.
Bi. Zainabu amesema vijana wengi nchini wanakumbana na tatizo la kuambiwa kuwa na uzeofu katika kazi kwa kipindi kisichopungua miaka kadhaa hali inayofanya wahitimu wengi kuelea kusota mitaani.
Aidha ameongeza kuwa nchi nyingi zimeweza kuandaa sera hizo ikiwemo nchi jirani za Kenya na Uganda na kusema endapo sera hiyo itafinyiwa kazi nchini basi tatizo hilo linaweza kupungua kama si kumalizika kabisa.
Aidha amesema kuwa licha ya kupata mafunzo hayo ambayo watayapata kupitia taasisi hizo pia yataweza kufungua soko la ajira kwa vijana wengi ndani na nje ya nchi.