Tuesday , 12th Apr , 2016

Klabu Bingwa ya mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es salaam inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi ya Aprili 16 mwaka huu Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam kwa kushirikisha jumla ya vilabu 14 vya wanaume na wanawake.

Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es salaam DAREVA Siraju Mwasha amesema, vilabu vilivyohakiki ushiriki wao ni 11 vya wanaume na vitatu vya wanawake ambavyo vimetakiwa kufika kwa muda ili kuweza kuanza michuano hiyo kwa muda unaotakiwa.

Mwasha amesema, kwa msimu huu watakuwa na ligi ya muda mrefu ambayo itahitimishwa mwezi Agosti mwaka huu wakiwa na lengo la kutaka mpira wa wavu kuendelea kuonekana zaidi kwa kila mwishoni mwa wiki mkoa wa Dar es salaam.

Mwasha amesema, mashabiki ndio wenye mchezo huo hivyo wanatakiwa kufika ili kuweza kuangalia na kuweza kutoa maoni yao ili kuweza kuukuza zaidi mchezo huo kwa mkoa wa Dar es salaam.