Monday , 28th Mar , 2016

Taasisi ya kibiashara toka nchini Thailand kwa Ushirikiano na Tanzania wametiliana saini ya Mkataba wa uzalishaji wa Umeme Jua mega wat 10 wenye thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 7.

Rais wa Taasisi za kibiashara toka nchini Tanzania Hamad Rashid Mohammed .

Akizungumzia kuhusu mradi huo ambao unatarajiwa kuanza Zanzibar katika kipindi cha miezi sita baada ya kufanya utafiti , Rais wa Taasisi za kibiashara toka nchini Tanzania Hamad Rashid Mohammed amesema lengo la kuanzisha maradi huo ni kutaka kuwapunguzia wananchi makali ya maisha hasa katika upatikanaji wa umeme nchini.

Hamad Rashid amesema teknolojia hiyo ambayo inamuwezesha mwananchi kutumia taa ambazo zinawaka zenyewe kwa muda wa masaa matano hata kama umeme umekatika zitarahisisha wananchi wengi kuweza kuzimudu visiwani humo.

Rais huyo wa Taasisi za Kibiashara ameongeza kuwa visiwa vya Zanzibar asilimia 90 ya wakazi wake wanatumia Mkaa na kuni na kusema kuwa ili kuondokana na tatizo hilo Wananchi wataweza kufaidika na mradi huo wa umeme jua ambao utawapungizia gharama zaidi.

Hamad Rashid amesema kampuni hiyo imeamua kuwekeza kwanza Zanzibar kulingana na mahitaji halisi ya Zanzibar katika suala zima la upatikanaji wa umeme wa uhakika halikadhalika kupunguza gharama kwa serikali ya Zanzibar.

Taasisi hiyo pia imetia saini mkataba mwingine wa uzalishaji wa dawa ambao umepanga pia kutumia malighafi za Tanzania kutengeneza dawa za binadamu ili kuona gharama za ununuzi wa dawa kwa Wananchi.

Hamad Rashid akielezea umuhimu wa uwekezaji huo wa Umeme