Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage
Akizungumza na waaandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage amawataka wadau wakiwemo wananchi wanaowafahamu wafanyabishara wanaoficha sukari wawafichue ili wawashughulikie.
Mhe. Charles amesema kwa taarifa ambazo serikali inazo mpaka sasa hakuna upungufu wowote wa sukari na kusema mfanyabiashara atakaebainika kuficha sukari serikali haitasika kuwafutia leseni zao.
Katika hatua Nyingine Waziri huyo wa viwanda amesema katika mchakato wa kufufua viwanda serikali imepanga kukirejesha kiwanda cha General tyre, na yatari serikali imekwisha chukua hisa aslimia mia moja na wako mbioni kuanza uzalishaji.