Wednesday , 24th Feb , 2016

Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika pambano la kuwania ubingwa wa mabara wa WBF utakaowakutanisha bondia namba moja nchini, Francis Cheka na bingwa wa ngumi kutokea bara la Ulaya, Geard Ajetovic ambaye amekwisha wasili nchini.

Rais wa ngumi za kulipwa nchini, TPBO, Yassin Abdallah ‘Ustadh’ amesema wameshajiandaa kwa ajili ya mpambano huo wa marudiano ambapo Cheka alipigana na Ajetovic mwaka 2008 ambapo Cheka kupoteza mpambano huo.

Ustadh amesema, mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kushuhidia mpambano huo ambao wanaamini Cheka ataibuka na ushindi n akuweza kuitangaza nchi.

Ustadh amesema, wameshamuandaa Cheka kwa ajili ya kushinda kwani wanajiamini wanaweza na ni mabingwa wa dunia hivyo wanafanya muendelezo wa kuongeza mabondia hapa nchini.