Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,Akizungumza jana Ikulu Jijini Dar es Salaam na Makundi ya Wanahabari, wasanii, Tehama na Chama cha mapinduzi
Akizungumza jana Ikulu Jijini Dar es Salaam na Makundi ya Wanahabari, wasanii, Tehama na Chama cha mapinduzi ambao walishiriki katika kupiga kampeni rais magufuli amesema kuwa serikali imepanga kufufua na kuanzisha viwanda laiki vilivyopo vina changamoto nyingi ambazo zinaweza kutatuliwa.
Rais Magufuli amesema viwanda vya sukari vinashindwa kuzalosha zaidi,kutoa ajira na kununua sukari kwa walima wa miwa na kulipa kodi kwa serikali kutokana na soko kujaa sukari kutoka nje.
Dkt. Magufuli ameongeza kuwa wakati mwingine sukari kutoka nje nyingine zinakua muda wake wa kuharibika umeshafikia na inapoletwa nchini tarehe husogezwa mbele kuonyesha inafaa kwa matumizi.
Aidha amewataka watanzania wote bila kujali itikadi,rangi, kabila wala dini wanatakiwa kuisaidia Tanzania kufikia uchumi wa kati kwa kukuza sekta ya viwanda itakayotoa ajira kwa na kukuza uchumi.