Muongoza video Inno Mafuru akiwa na Chabba, Kala Jeremiah na ROMA
Akiwa ametumia majina kibao ya mastaa wanaowika bongo, kitu ambacho kimepokelewa tofauti, Chaba amefafanua kuwa hiyo ni njia rahisi ya kuwaelewesha mashabiki juu ya kile anachotaka kusema kutokana na mastaa hao kufahamika vizuri katika kona za mitaa.
Mastaa wanaosikika katika rekodi hiyo ya Chaba ni kwa sehemu kubwa ni kutoka bongo movie akiwepo Batuli, Riyama, Irene Uwoya kati ya wengine wengi.
Staa huyo amesema kuwa, kazi hiyo nzuri imefanyika chini ya Cyne Studio kutoka Arusha huku rapa G Nako aliyemshirikisha katika kazi hiyo akiwa hajatokea kutokana na ratiba kupishana kidogo.