Saturday , 2nd Jan , 2016

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema hatarajii kuwaona Makatibu wakuu na Manaibu makatibu wakuu wanakua na kigugumizi katika kuchukua maamuzi dhidi ya watumishi watakao kuwa na makosa.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue

Akizungumza kabla ya kuwasilshwa kwa mada katika semina Elekezi ya Makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu hao Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa haitakubalika kwa mtumishi aliefanya kosa katika sehemu moja kuhamishiwa sehemu nyingine badala ya kuchukua hatua palepale.

Aidha ameongeza kuwa serikali ya awamu ya tano inatarajia viongozi hao kuwa watakuwa wasimamizi wazuri wa fedha za umma na kwamba haitarajii kuwepo kwa hati za ukaguzi za mahesabu zenye kasoro.

Balozi Sefue ameongeza kuwa viongozi hao wanapaswa kujua nafasi yake ni ya maamuzi hivyo serikali inatarajia kuona daima anafanya maamuzi kwa usahihi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazomuongoza katika majukumu yake.