Tuesday , 29th Dec , 2015

Mvua iliyoambatana na upepo mkali imeleta maafa katika kata ya Ikuti wilayani Rungwe mkoani Mbeya baada ya kuezua nyumba 23 na kuangusha migomba yenye tahamani ya zaidi ya shilingi milioni 250.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, Abasi Kandoro ametembelea waathiria wa mvua

Mvua hiyo iliyonyesha kwa muda mfupi na kuleta madhara makubwa ilimlazimu mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, Abasi Kandoro kutembelea waathirika wa mvua hizo.

Akiongea na viongozi wa eneo hilo Bw. Kandoro amewataka viongozi hao kuitisha mikutano ya dharura ili kujua ni jinsi gani ya kutatua changamoto ya tatizo hilo ikiwemo kuwasaidia waathirika wa majanga hayo.

Akitoa taarifa ya madhara ya mafuriko hayo afisa kilimo wa wilaya hiyo Godwin Katiko ambapo amesema katika kaya mia moja zilizoathiriwa jumla ya milioni 253 zingeweza kupatikana kwa ajili ya kilimo cha ndizi na shughuli nyingine za kimaendeleo.