Wednesday , 23rd Dec , 2015

Chama ha Gofu nchini TGU kimelalamikia ukosefu wa makocha wa timu ya taifa wenye viwango vya kimataifa.

Mwenyekiti wa TGU Joseph Tango amesema, wakati chama kikihangaika kuhakikisha wachezaji wake wanafuzu kucheza michuano ya dunia bado kinakabiliwa na ukosefu wa fedha za kumwajiri kocha wa kimataifa atakayekuwa na uwezo wa kuinoa timu ya taifa.

Tango amesema, mipango ya TGU ni kuhakikisha Julai 19 hadi 24 mwakani Tanzania inapeleka wachezaji katika mashindano ya dunia ya vijana chini ya miaka 16 lakini ingekuwa vizuri kama wachezaji hao wangepata kocha wa kimataifa kutoka nje ya nchi.

Tango amesema, licha ya wachezaji wa timu ya taifa kufanikiwa kufanya vizuri katika mashindano yote ya vijana mwaka huu lakini huenda matokeo hayo yangekuwa bora zaidi endapo makocha wazawa wangepata kocha mwingine kutoka nje ya nchi mwenye viwango vya kimataifa.

Katika mashindano hayo yatakayofanyika nchini Scotland kila taifa linatakiwa kupeleka wachezaji wawili wa kike na wa kiume waliofuzu viwango vya dunia.