Tuesday , 22nd Dec , 2015

Wilaya ya Arumeru inakusudia kuanzisha operesheni maalumu ili kubaini wamiliki matapeli wa mashirika yasiokuwa ya kiserikali yaliyopo wilayani humo, wanayodaiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya taifa.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Wilson Nkambako.

Akizungumza katika uzinduzi wa mafuzo ya mashirika yanayojiendesha bila faida wilayani Arumeru, Mkuu wa wilaya ya Arumeru Wilson Nkambako amesema serikali haitalifumbia macho swala hilo kwa baadhi ya watu kujipatia fedha kwa ujanjanjaujanja .

Joshua Nasary ni mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki ambae amebainisha kuwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ni wadau wakubwa wa maendeleo iwapo yatatumika vizuri, licha ya kuwa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kuzisaidi hazitoshi ikilinganishwa na mahitaji yake.

Nae Mkurugenzi wa kituo cha maendeleo na ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Denmark cha MS-TCDC kilichopo Jijini Arusha Dakta Suma Kaare, amesema utafiti umebaini asilimia kubwa ya misaada inayotolewa kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali haiwafikii walengwa ambao ni wanajamii.

Dakta Suma ameongeza kwamba hali hiyo inarudisha nyuma jitihada za kuibadili Afrika ambayo hata hivyo sio vyema sana kuendelea kusubiri misaada kutoka nje na badala yake inapaswa kujitegemea yenyewe kwa kutumia rasilimali ilizonazo.

Mafunzo haya yanayotelewa kwa wamiliki wa mashirika na taasisi zinazojiendesha bila faidi kwa miaka mitatu ni yakwanza kufanyika katika ukanda wa AFRIKA yanayotelewa na kituo cha MSTCDC.