Thursday , 17th Dec , 2015

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi, ajira, vjana na watu wenye ulemevu Mh. Jenista Mhagama ametaka apelekewe ripoti ya matuzimizi ya sh. Milioni 700 ya ujezi wa daraja maeneo ya Ununio Jijini Dar es salaam

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, anaeshughulikia sera,uratibu na Bunge,Kazi ,ajira, vjana na watu wenye ulemevu Mh. Jenista Muhagama.

Waziri Jenista ametaka ripoti hiyo baada ya jana kufanya ziara katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ili kujua chanzo cha tatizo hilo na kugundua kuna ubadhirifu wa fedha baada ya miundombinu mingi kujengwa chini ya kiwango.

Bi. Jenista ametaka wakandarasi waliopewa tenda hiyo pamoja na viongozi waliopuuza maagizo ya serikali katika utekelezaji wa utengenezaji wa miundo mbinu hiyo kuchukuliwa hatua ili kuokoa fedha za watanzania na hasara wanazokutana nazo kipindi cha mvua.

Mei mwaka huu Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete alitoa agizo la kubomolewa kwa gereji ya MSK, iliyoko eneo la Boko Basihaya ili kupisha mkondo wa maji yanayosababisha wakazi wa eneo hilo kukumbwa na mafuriko wakati wa mvua.

Katika hatua nyingine Mh. Jenista amemtaka mkurugenzi wa manispaa ya Ilala kusitisha mkataba wa mkandarasi anayejenga mtaro wa Kwa Mnyamani Buguruni kwa kuwa anajenga chini ya kiwango na kuendelea kusababisha mafuriko.